Mambo muhimu ya kuyafahamu
1. Kware aina
ya Japanese ni kware anaefugwa ndani ya uzio na katika banda la wavu.
2. Si vizuri
aishi na kinyesi chake.
3. Kware aina
ya japanese ni tofauti na kware wa porini anaepatikana Tanzania.
Chakula.
1. Kware
anakula chakula chochote anachoweza kula kuku ikiwemo chakula cha broiler. Kama
utaamua kuwapa chakula cha broiler unawapa “starter” kware wenye umri kuanzia
siku moja hadi wiki ya tatu baada ya
hapo unawapa Falcon au hill.
2. Ukiweza
kuwatengenezea chakula chako mwenye kutumia pumba nk. Ni vizuri zaidi kwa mayai
yenye lishe 100%
3. Kware 100
wenye umri wa mwezi hutumia kiroba cha kilo 20 kwa wiki 3.
4. Kware
hawamalizi chakula kama kuku.
5. Pia kware
hupewa majani kama mchicha nk.
Magonjwa:
1. Kware hawa
hawasumbuliwi na magonjwa bali hudonoana tu wenyewe endapo watawekwa wengi
katika sehemu ndogo. Hivyo ni lazima uwe na majani ya aroevela karibu kwa ajili
ya kuwapaka maji yake pale wanapoumia.
ZINGATIA:
Wanapokosa madini ya kutosha kwenye chakula huweza kupata
madhara yafuatayo:-
1. Kuharisha
2. Kunyonyoka
manyoya
3. Kupunguza
kasi ya kutaga mayai.
nimefulaishwa na somo nzuri
ReplyDeletenimefulaishwa na somo nzuri
ReplyDeletehabari za kazi, samahani nimevutiwa sana na ufugaji wa kware. sasa kwa hapa Tanzania naweza kuwapata wapi?
ReplyDelete