
Leo ningependa niingie ndani kuwa nini hasa tofauti ya mayai ya kware na yale ya kuku ingawa taarifa nyingi nilizopata kwenye mitandao na kwinginekoinaonyesha tu kwa habari za watu waliopata kutumia mayai kware na kuona umuhimu wake katika afya na baadhi ya tovuti kuongelea tu kwamba mayai haya ni mazuri yanasaidia kwa afya bado kama watu wanaotaka kueleew inakuwa haikidhi haja kuamani tu yakuwa yana saidia katika afya, nikiwa mmojawapo wa watu ambao niliona yanasaidia watu walikuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakiendelea vizuri.
Na mpaka sasa mimi napenda kukiita hiki chakula bora na sio dawa kama watu wengi waliotumia wakapata nafuu kwa yale waliokuwa yakiwasibu na wale waliokuwa na dhaifu nyingine katika mwili wakarejea afya maridhawa lakini msimano wangu binafsi napenda kutambua mchango wa haya mayai kama chakula bora.

Katika kutafuta nikasema pamoja na vyanzo vya wataalamu binafsi ningependa kupata vyanzo vilivyo vya kiserekali ambavyo wao hawana upande waliolalia maana hawa wataalamu binafsi wanaweza kuwa na ajenda zao, Na ndipo nilipopata utafiti wa USDA (United State Department of Agriculture) unaonyesha tofauti za mayai haya kwa kina katika category 78 za nutrients zilizogawanya mayai ya kware yana vitu 31 zaidi ambayo ya kuku hayana kabisa wakati yale ya kuku ya kitu kimoja tu ambacho hakiko kwenye ya kware ambacho naomba nikitaje nacho ni Vitamin K (phylloquinone) na katika hizo 45 vilivyobaki vya kware 42 viko juu na vingine hata mara mbili ya zile za kuku, wakati vya kuku ni 3 vitatu ambayo vimezidi vile vya kware. Angalia link hizo hapo chini kwa number kamili
Faida hizi zote tunaweza kupata kama watu wetu watajiingiza katika ufugaji wa ndege huyu ambaye anapatikana sehemu nyingi unaweza kuanza kidogo kidogo mpaka wakafikia wengi,na kama unavyooana hapo juu unaweza kutengeneza banda rahisi la mbao laini na wafu na kuanzia hapo, ila wawapo wadogo waweke kwenye box na kuwawekea taa kama ufanyavyo kuku.
Ufugaji nyuma ya nyumba