Ads (728x90)

Biashara yetu ni kuhusu kware tu. Ujue mfugo unaoshika hatamu katika miaka hii. Mfugo unaoweza badilisha maisha yako. 

Kware ni ndege mdogo mwenye asili ya toka huko Japan. Wakiwa mwituni kware ni ndege wanaohama hama na kuishi mashambani. Rangi ya kware huyu wa mjapan ni yenye madoadoa ya brown meupe na meusi yanayoanzia kichwani mwake na hadi mkiani tumboni kware akiwa light brown. kware pia wanapatikana katika rangi tofauti kama nyeupe tupu, au nyeupe na nyeusi, Kware mkubwa anapatikana katika sentimita 20 (7 ¾ Inch)  kwa urefu na gram 150 kwa uzito. 

Ufugaji wake ulianza toka karne ya 14, mwanzoni walijulikana kama ndege wa mbugani lakini ufugaji wao na umaarufu umetokana na utamu wa mayai yake na nyama. Miaka ya 1910 waliwagawa kware katika makundi ya kware wa mayai na kware wa nyama hapo lakini siku hizi kware sio ndege maarufu kama wengine mfano kuku lakini kware anahitaji kujulikana zaidi kutokana na faida zake.

Kware wanaweza kufugwa katika banda dogo na katika eneo la mita moja ya mraba unaweza kuwatunza kware hadi 20 na hawa wanaweza kutaga mayai ya kutosha familia yenye watu wanne. Ufugaji wa kware wachache haina changamoto na kware wanapenda kukaa chini sio ndege wapendao kuruka na kuninginia juu. 

Wakiwekwa katika banda lenye hali ya joto 16ºC (61º F) , uwepo wa nafasi na chakula cha kutosha kware mmoja anataga mayai 280 au 290 kwa mwaka.

Kware wa kufungwa hatengenezi kiota kwa hiyo hawezi kulalia mayai yake kwahiyo kuwaongeza utahitaji ku-incubate mayai yao. Kware ataanza kutaga mayai akifikisha wiki ya saba na hutaga mayai kwa kipindi cha meizi 15 - 16 ikitegemea mazingira yanayoshauriwa kwa ufugaji.

Mbali na kuliwa na binadamu mayai ya kware huchemshwa au kunywewa kama dawa kutokana na kuwa na vitamini nyingi kuliko mayai mengine.

Kama unapanga kufuga kware soma makala zaidi katika blog hii uweze kujua kila kitu na kuuliza maswali. 

Post a Comment

  1. Mayai ya kware yanaweza kukaa kwa muda gani bila ya kuharibika na kufaa kuliwa? Mazingira gani yanayofaa kuhifadhi mayai ya kware kwa muda mrefu inavyowezekana?

    ReplyDelete